Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anahitaji kupata usaidizi wa kutosha kutoka kwa viongozi na hasa wasaidizi  kuanzia ngazi ya nyumba kumi hadi taifa.

Maneno hayo yametamkwa na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba alipofanya mahojiano na Idara ya Habari – MAELEZO – ofisini kwake Oysterbay Jijini Dar-es-Salaam.

Jaji Warioba ameona kuna udhaifu mkubwa wa kiutendaji ambapo wananchi hawatoi changamoto zinazowakabili mpaka wamuone Rais amefika katika eneo lao, au wanaeleza changamoto zinazowakabili kwa viongozi husika ila, viongozi hawazifanyii kazi, ambapo wananchi wanaamua kuziwasilisha kwa Rais mara wanapomuona.

 “Rais hawezi kufanya kazi peke yake naomba tuimarishe utendaji wetu wa kazi, kama utendaji ungekuwa mzuri suala la makontena kufika hadi bandarini lisingekuwepo, na hata kugundulika kwake kusingefanywa na Rais,” amesema Jaji Warioba.

“Nampongeza sana Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na  Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa, kwa utendaji wao wa kazi. Viongozi hawa ni wasikivu na wanatekeleza kazi zao bila mihemko kwa kutoa maagizo na maelekezo kwa wahusika ili wayatekeleze”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *