Kundi la muziki wa Taarab nchini, Jahazi Modern Taarab linatarajia kufanya onesho litakalofanyika katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam siku ya Agosti 20 mwaka huu.

Meneja wa ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo amesema kwamba usiku huo Jahazi wataimba nyimbo zao zote kali mpya na za zamani zinazobamba wakiwa na wakali kama Leyla Rashid, Fatma Shobo, Rahma Machupa, Fatma Kassim na wengine kibao.

wape

Pia Mbizo amesema usiku huo utakuwa wa toa kitu weka kitu, Jahazi kama wanavyojulikana siyo watu wa kubahatisha ambapo zitaimbwa nyimbo kama Mahaba Niue, Nina Moyo Siyo Jiwe, Nia Safi Hairogwi, Kamwe Sitaumbuka, Kaning’ang’ania Mpenzi Chocolate na nyingine nyingi.

Vile vile kwa mara ya kwanza wakali wapya kwenye kundi hilo kama Aisha Vuvuzela na Zubeda Mlamali watalivamia jukwaa kwa kutoa burudani kwa wapenzi watakaojitokeza katika onesho hilo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *