Kundi la muziki wa Taraab nchini, Jahazi Modern Taarab leo linatarajia kuwasha moto mkesha wa Krisimasi katika ukumbi wa burudani Dar Live uliopo maeneo ya Mbagala jijinini Dar es Salaam.

Katika show hiyo Jahazi watasindikizwa na mkali wa Singeli nchini Msaga Sumu ambaye nae atatoa show ya kufa mtu kwenye ukumbi huo maarufu jijini Dar es Salaam,

Meneja wa ukumbi wa Dar Live na Jahazi, Juma Mbizo amesema kuwa kundi hilo leo litafanya show ya kufa mtu ambayo pia itawadondosha wasanii nyota wa muziki huo waliowahi kuwika na bendi mbali mbali kama vile Ally Jay na Mosi Suleimani.

Mbizo amesema kuwa kiingilio kwenye show hiyo itakuwa shilingi 7,000 hivyo amewataka mashabiki kuja kwa kwa wingi kuja kupata burudani kutoka kwa kundi hilo linaloongozwa na Leila Rashid pamoja na Amigo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *