Mwanamuziki maarufu nchini Kenya, Charles Njagua maarufu kama Jaguar ameshinda Ubunge jimbo la Starehe nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika jana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Jaguar amewashukuru wananchi wa jimbo hilo huku akisema kuwa bila wao asingefanikisha hilo, huku akiwashukuru wapinzani wake kwa kukubali ushindi wake huo.

Ameandika “Hakuna linalowezekana bila Mungu, Nawashukuru watu wa Starehe kwa ujasiiri na kuniamini kuwawakilisha bungeni, nawashukuru wote walioniunga mkono , marafiki, familia ambao walikuwa nami wakati wa kampeni.

Ameendelea kuandika ‘Pia nawampongeza mpinzani wangu Steve Mbogo, Boniface Mwangi na Mh. Kwenya ambao waliweka kampeni safi.

Pia ameandika ‘Huu sio ushindi wa Starehe tu bali ni ushindi wa vijana wote nchini Kenya ambao wameona mbele, sasa tuijenge Starehe ile tunayoitaka, Mungu awabariki”.

Jaguar ameibuka mshindi wa Jimbo hilo kwa asilimia 53% ya kura zote, huku akifuatiwa na Steve Ndwiga  aliyepata asilimia 31% na Boniface Mwangi akipata aliyepata asilimia 13%.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *