Mwanamuziki wa Genge nchini Kenya, Jaguar amekana shitaka la kusababisha vifo vya watu wawili vilivyosababishwa na gari lake.

Jaguar amefikishwa katika mahakama ya Baricho iliyopo eneo la Kirinyaga baada ya uchunguzi wa ajali iliyosababishwa na gari lake kuendelea kwa wiki tatu sasa.

Mwanamuziki huyo alifikishwa mbele ya hakimu mkazi na kujibu shtaka la kusababisha vifo vya vijana wawili wa bodaboda kufuatia ajali iliyohusisha gari lake aina ya Range rover spot nchini Kenya.

Mwanamuziki Jaguar wa kwanza kushoto waliokaa akiwa mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayomkabili.
Mwanamuziki Jaguar wa kwanza kushoto waliokaa akiwa mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayomkabili.

Hapo awali Jaguar alijaribu kufanya ‘cover up’ kwa kuandikisha ripoti iliyotofautiana na kile walichosema mashuhuda wa ajali hiyo.

Jaguar amekana shtaka hilo na kuachiwa kwa dhamana la shilingi laki moja ya kenya ambapo kesi hiyo itatajwa tena Juni 8 mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *