Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa hana haja ya kuingia tena kwenye mahusiano ya kimapenzi baada ya kuachana na Harmonize.

Wolper amesema kuwa wanaume wengi wenye fedha wamekuwa wakimsumbua kumtaka kimapenzi lakini haoni haja ya kuwa nao kwa kuwa anaamini ni wasumbufu tu hawana mapenzi ya kweli.

Kauli hiyo ya muigizaji huyo imekuja siku kadhaa baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize kutoka WCB.

Mkali huyo wa movie za Bongo amesema kuwa kutokana na upendo wa kweli anaojitahidi kumuonyesha mwanaume anapokuwanaye kwenye uhusiano na kujikuta akiambulia maumivu.

Wolper amesema kuwa kwasasa hana mpenzi ameona bora aweke pembeni mambo ya mapenzi na ajikite kwenye kazi zake na biashara zake.

Jacqueline Wolper alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Harmonize ambapo kwasasa wameachana huku Harmonize akiwa na mwanamke mwingine ambapo ana ujauzito na anatarajia kupata mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *