Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amfungukia mpenzi wa Sarah ambaye ni mpenzi wa Harmonize kuwa yeye ndo alimuachia Harmonize kwaiyo siku yoyote akimtaka atamchukua tena.

Miezi michache iliyopita Wolper aliweka wazi kuwa walipokuwa kwenye uhusiano na Harmonize, ex wake huyo alianza kuchepuka na mzungu Sarah kutokana na kipato chake kikubwa yaani Sarah alikuwa anamhonga Harmonize ili awe naye na amuache Wolper baada ya kutambua hilo Wolper ndo alikuwa wa kwanza kumuacha Harmonize na baada ya hapo Harmonize akaweka hadharani mahusiano yake na Sarah.

Tangu hapo Wolper na Sarah wamekuwa wakijibishana kwenye mitandao ya kijamii. Siku ya jana Srah alweka hadharani maongezi baina yake na Wolper waliyoyaongea faragha keen he maongezi hayo Wolper aliweka wazi kuwa endapo Sarah ataendelea kumfatilia basi atamchukua Harmonize kutoka kwenye mikono yake.

Tafadhali usinitafute ongea na mwanaume wako we ni chizi nini? Alihoji Wolper kwenye meseji hizo, Unanitafuta tena Sarah? Sema ndio uone nitakacho kufanyia! Siwezi kuwa na Harmonize ila ukiendelea kunifuata fuata nitamchukua. Mimi ndio nilikupa nafasi wewe use naye kwaiyo usije ukafikiria hata kwa sekunde kuwa ntasita kumchukua tena, mimi ndo nilikuachia uwe naye na nikimtaka vile vile namchukua! Aliandika Wolper.

Baada ya mazungumzo hayo kuvuja wapo watu wengi waliodai kuwa aliyesambaza meseji hizo siyo mwengine bali ni Harmonize ili tu apate kiki ya wimbo wake mpya alioutoa juzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *