Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka kwa kuwachana baadhi ya watu wanaofuatilia maisha yake.

Wolper ameamua kusema hayo kutokana na watu kumfuatilia maisha yake baada ya kupata mpenzi wake mpya anayefahamika kwa jina la Brown.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wolper ameamua kutoa ushauri kwa watu hao wanaopenda kufuatilia maisha yake.

Wolper ameanza kwa kuandika kuwa “Basi leo nataka niwaambie kitu hakuna binadamu anaependa hivyo ww ulivyo na ndio maana unakuta wanazua mambo mengi ili wajaribu kukufanya ujione mdhaifu,Binadam bwana wanaweza wakatafuta tatizo pasipo kuwa na tatizo!”

Ameendelea kuandika kuwa “Wakiona mtu yupo happy anajitafutia,anafanya yanayo muhusu wanaona hilo ni kosa na mbaya zaidi wakigundua una furaha wanajaribu kukufanya uwe down,Ingawa sio wote lkn wapo hawa watu na wengine tupo nao majumbani mwetu tunaishi nao.

Pia ameandika “Unakuta mtu unafanya kitu kizuuuri lkn haupongezwi kwa lolote mbaya zaidi wanakiponda ili ujikatie tamaa na hiyo yote kwasababu wao hawana basi wanataka ww uwe km wao…Sasa niwashauri ndugu zangu tusiwe watu wakuchulia kitu km kilivyo kuna wengine wanataka kukuona tu umeshindwa hiyo ndo furaha yao wao,fanya mwenyewe,amua mwenyewe na pia jipongeze mwenyewe ikiwezekana nyamaza kabisa wasijue yako ila wape nafasi ya kuona mafanikio yako..

Mwisho amemalizia kwa kuandika “Usikubali kumpa mtu mwingine nafasi zaidi ya ww unavyotakiwa kujipa..Jipe nafasi,Jipongeze na jiamini bila kujali mwingine anasema au atasema nn…Pambana na uwezo wako cha msingi usishindane nao…Amini unaweza kupitia wewe mwenyewe!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *