Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amethibitisha kuachana na mpenzi wake mwanamuziki Harmonize kutoka lebo ya Wasafi.

Muigizaji huyo aliweka wazi kuwa hayupo tena kwenye mahusiano na muimbaji huyo wa wimbo kwasasa na kila mtu ana fanya mambo yake.

Jacqueline Wolper amesema kuwa habari zinazoenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wapo pamoja siyo kweli kutokana na kila mtu ana mambo yake kwasasa.

 Mklai huyo amesema kuwa una watu wengi anapokea simu zao na wengine wameenda hadi dukani kumuuliza kuhusu habari hizo za ukweli au siyo za kweli kutokana na habari za kuwa pamoja kuzagaa sana katika mitandao ya kijamii.

Pia amesema kuwa  “Yaani nawaapia mimi kitu kidogo naweza kikanikaba rohoni nikawa naumia muda wote. Halafu ikishakuja kwenye maumivu siwezagi tena drama, naongeaga ukweli hata uwe wa aina gani, mashabiki zangu nyie mashahidi ninaelezeaha story nzima pasipo kuficha japo yaweza kuwa na aibu ama vitu nilivyokua navumilia yakinishinda naongeaga. Kwa sasa hivi naugulia moyoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *