Baada ya kusambaa kwa taarifa za muigizaji wa Bongo Movie, Miriam Jolwa maarufu kama jini Kabula kuwa amechanganyikiwa kiakili, hatimaye muigizaji mwenzake Jacqueline Wolper ameonyesha kuguswa na tatizo hilo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Jacqueline Wolper ameonesha jinsi gani amesikitishwa kuugua kwa muingizaji huyo maarufu nchini.

Jacqueline Wolper ameanza kwa kuandika ”Kabula wanguNatamani niongee mambo mengi sana juu yako lakini natamani ata kukusaidia urudishe akili yako swali ni kwamba nimechelewa??nakama nimewahi je nitafanikiwa kwelisasa tuzungumze jambo jamani maana siju hizi tarfa tunazipata insta naona nalangu niliongelee insta wanatasnia wenzangu tunamsaidiaje mwenzetu nini kimekuta kipi je nayoyasikia ndio hayo????nakama ndio mbona kuna wataalam wakusena nae naakakaaa sawa.

Pia ameongeza kwa kuandika “Basi watanzania wenzangu naombeni tuchangie maoni yenu hapa nakama nim2 uwezi toa ushauri hapa basi tuma msg kwakupitia cm hii 0765776776 basi tuweze kumrudisha kabula jamaninaandika msg hii huku nalia namoyo mdogo sana usiweza kuvumilia naumivu nakumbuka nimishawahi kumwambia kabula we nimwanamke mzuri sana bongo movie lkn natamani kujua tatizo nini kacheka tuu akachukua nguo akaondoka sikupata muda wakuzungunza nae.

Mwisho amemalizia kwa kuandika kuwa “Sasa npo safarini hope kesho au kesho kutwa nikijaliwa tukutane kwaomoja .. Bongo movie tumfwate alipo jamani tujue tunamsaidiaje nimeona video anaongea sjui niamechanganyikiwa masikn me ata nashindwa kuandika jamani.”.

Kabula ambaye alitamba miaka ya nyuma kwenye tamthilia ya Jumba la Dhahabu akiigiza kama jini amekumbwa na matatizo ya akili bada ya kuchanganyikiwa ambapo anaongea mambo yasioleweka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *