Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa amehama Chadema kutokana na viongozi wa chama hicho kushindwa kutambua mchango wake wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Wolper amefunguka hayo baada ya kuulizwa swali katika mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini na ubainisha hayo.

Muigizaji huyo alikuwa miongoni mwa wasanii wa Bongo Movie waliojitoa kupiga kampeni katika Chama cha Chadema kwenye uchaguzi mkuu uliopita lakini akaamua kuhama ndani ya Chama hicho na kuhamia CCM.

Amesema hajawai kuwa msaliti kwani hakuwa mwanachama wa chama hicho lakini alisikitishwa na uongozi wa chama kushindwa hata kumshukuru kwa kazi aliyoifanya wakati wa uchaguzi mkuu kwa kujitoa pasipo kulipwa hata shilingi elfu 10 za kitanzania.

Pamoja na kuwa alifanya kampeni za kumsapoti Mgombea uraisi kupitia mwamvuli wa UKAWA Edward Lowassa, Wolper amedai kuwa hakuwa anasapoti chama kizima bali mgombea kwa kuwa yeye ni shabiki wa kiongozi huyo na familia yake kwa ujumla ndiyo maana hakukubali kulipwa katika kampeni hizo.

Pia Wolper amekiri wazi hata tatizo na Lowassa na hawezi kumlaaumu kwa yaliyotokea bali atakuwa naye bega kwa bega tena kumsapoti endapo atapata tena nafasi ya kugombea urais 2020.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *