Muigijzaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka ya moyoni kwa kusema kuwa amewaachia penzi la Harmonize wajuaji ambao walitka waachane.

Wolper amesema kuwa baada ya kumwagana na Harmonize kwa sasa ameamua kujikita zaidi katika kufanya mambo yake ya kimaendeleo.

Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema kuwa mambo ya mapenzi na msanii huyo wa Bongo Fleva amewaachia wajuaji ambao anaamini walikuwa wakimtolea macho kitambo wakati wapo kwenye mahusiano.

harmonize

Wolper amesema kuwa “Harmonize nimewaachia wajuaji wawe naye, nimeamua kuwa bize na mambo yangu ya maendeleo zaidi, suala la mapenzi nimeliweka pembeni kwanza,”.

Muigizaji huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize kutoka WCB ambao kwasasa wameachana rasmi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *