Muigizaji wa Bongo Movie, Jackline Wolper amesema kuwa  uhusiano wa wasanii wenzake, Aika na Nahreel, wanaounda kundi la muziki la Navy Kenzo, ndiyo ‘couple’ imara zaidi kwa wasanii kwa sasa.

Wolper amesema anafurahishwa na wanavyoweza kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo katika uhusiano wao na hawayumbishwi licha ya kuwa mastaa wakubwa kwa sasa katika muziki.

Navy kenzo

Wolper ambaye kwa sasa yupo kwenye uhusiano na msanii kutoka kundi la WCB anayejulikana kwa jina la Harmonize, amesema uhusiano wa wasanii hao unampa funzo kubwa katika maisha yake ya uhusiano huku akiahidi kufuata nyayo zao.

Wasanii wapenzi hao wanaounda kundi la Navy Kenzo, walinukuliwa hivi karibuni wakisema kwamba wanapokwazana na kutaka kuachana hufikiria ugumu waliopitia walipokuwa wakitengeneza majina yao na namna watakavyokuja kuyapoteza kirahisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *