Muigizaji maarufu wa filamu, Jackie Chain anatarajia kupokea tuzo ya heshima ya Oscar kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu duniani.

Wengine walioidhinishwa kupewa tuzo hizo za Oscar ni mhariri Anne Coates, muongozaji wa filamu, Lynn Stalmaster na mwandalizi wa filamu za makala Frederick Wiseman.

Rais wa jopo litakalotoa tuzo hizo, Cheryl Boone Isaacs amewataja wanne hao kama waasisi halisi na stadi katika kazi waliyoifanya.

Jackie Chan mwenye umri wa miaka 62 ni mwigizaji nyota katika filamu nyingi za kung-fu zilizoandaliwa katika nchi yake ya kuzaliwa Hong Kong.

Muigizaji huyo aliwahi kutamba kimataifa kwa filamu maarufu kama vile Rumble in the Bronx, Rush Hour na filamu ya vibonzo ya Kung Fu Panda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *