Mkali wa filamu za mapigano, Jimmy Mponda maarufu kama J Plus ameingiza sokoni filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘The Foundation’.

Ujio wa filamu hiyo inavunja ukimya wa staa huyo baada ya kukaa kimya kwa miaka minne bila kutoa filamu yoyote.

Kwenye filamu hiyo amewashirikisha waigizaji kibao akiwemo bingwa wa filamu hizo za mapigano Sebastian mwanangulo maarufu kwa jina la Inspekta Seba.

J Plus amesema kuwa anaaamini kuwa wapenzi wake walipenda sana filamu zake zilizo pita kama vile ‘Misukosuko’ Shamba kubwa.

Vile vile muigizaji huyo amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuinunua filamu hiyo kutokana ameitendea haki kama filamu zake zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *