Mwanamuzi nyota wa Marekani, Jennifer Lopez ‘J Lo’, amesema kuwa maisha magumu aliyoishi katika familia yake ndiyo yamemfanya ajitume zaidi katika kazi zake za muziki mpaka kufanikiwa.

J Lo ameweka wazi kuwa ametokea katika maisha ya kimasikini sana, ndicho kilichompa moyo wa kutaka kuwa tajiri.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 47, kwa sasa anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola milioni 300 ambazo ni zaidi ya bilioni 654 za Kitanzania.

Mwanamuziki amesema kuwa ni wazi kwamba ametokea katika maisha ya kimasikini, labda angetokea katika familia ya kitajiri asingekuwa JLo mpambanaji.

Pia ameongeza kuwa alikuwa anavaa kiatu kimoja kwa muda mrefu, jambo ambalo hatolisahau katika maisha yake lakini kwa sasa ana furaha kwa kuwa anafanya anachokitaka na anachokipenda kutokana na kuwa mali nyingi.

Mwanamuziki huyo ni miongoni mwa wanamuziki wakongwe nchini Marekani ambao wamepata mafanikio makubwa kutokana na kazi zake za uimbaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *