Mkali wa hip hop kutokea pande za Mbeya, Izzo Business amesema kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki mwenzake wa kundi la Amazing anayeitwa Abella.

Izzo amesisitiza juu ya uhusiano uliopo kati yake na msanii Bella ambaye kwa pamoja wameunda kundi la The Amazing na kusema hakuna uhusiano wowote wa kimapenzi.

Izzo B amesema kuwa alikutana na binti huyo ambaye amekulia Marekani kwenye mtandao wa kijamii lakini mahusiano makubwa yaliyopo kati yao ni kikazi tu na siyo kama wengi wanavyodhani kuwa ni wapenzi.

Kundi hilo kwasasa limeachia video  mpya inayokwenda kwa jina la ‘Umeniweza’ ambayo inafanya vizuri katika vituo mbali mbali vya radio na TV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *