Mwanamuziki wa Hip Hop nchini, Izzo Bizness amesema kundi lao ‘The Amazing’ limejipanga kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikiyakabili baadhi ya makundi ya muziki hapa nchini.

Izzo amesema kuwa kabla ya kuunda kundi hilo walikaacha chini na kuangalia namna ambavyo wataweza kukabiliana na matatizo yanayosababisha makundi mengi kuvunjika hapa nchini.

Pia rapa huyo amesema muziki kwa sasa umebadilika na kuwafanya wasanii kuacha kutegemea show pekee bali kujazatiti kwenye utoaji wa nyimbo bora kuliko kutegemea show tu.

Kundi hilo linaundwa na wasanii wawili ambao ni Izzo Buzness pamoja na Abela ambapo limeanza siku si nyingi na linabamba masikioni mwa watu baada ya kutoa nyimbo zao mpya.

Izzo ameongea hayo baada kuonekana makundi mengi ya muziki hapa Bongo yanavunjika kutoka na maslai miongoni mwa wasanii wanaonda makundi hayo kwa mfano Wanaume Family, East Coast Team, 2Berry na mengine mengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *