Mkali wa Bongo Fleva kutoka pande Green City, Izzo Bizness amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya kwa wasanii ndiyo chanzo cha kushusa uwezo wa baadhi ya wanamuziki nchini.

Izzo Bizness, anayetamba na wimbo wa ‘Umeniweza’ ameweka wazi kwamba dawa za kulevya ndizo zilizoshusha viwango vya baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaamini wasanii wengi wa muziki huo wameshuka viwango vyao vya kuimba na kutunga kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Izzo Bizness ametoa ushauri kwa kusema kuwa anawaasa wasanii wenzake kwa kusema  dawa ndizo zinazopunguza nguvu kazi za vijana na kuondoa thamani ya utu wao kwa jamii, ni bora waachane nazo kwa faida yao na nchi kwa ujumla.

Kauli ya Izzo Bizness imekuja kufuatia baadhi ya wanamuziki ambao walikuwa wana vipaji vya hali ya juu lakini wameshukua kimuziki kutokana na matumizi ya dawa za kulevya ambapo baadhi ya wasanii wamekiri kutumia dawa za kulevya.

Mwanamuziki TID  alikiri kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya mbele ya mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ulifanyika kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *