Mwanamuziki nyota wa Bongo Movie, Izzo Bizness amesema kuwa hana mahusiano na mwanamuziki mwenzake Abela ambaye wanaunda kundi la  ‘The Amazing’.

Kauli ya Izzo imekuja kufuatia baadhi ya mashabiki wakisema kuwa wawili hao wanamahusiano kutokana na ukaribu wao toka kuanza kwa kundi hilo ambalo kwasasa linafanya vizuri.

Izzo Bizness amesisitiza kuwa yeye ana mtu wake na Abela ana mtu wake hivyo siyo rahisi kuwa kwenye mahusiano wakati wanajuana vizuri kwamba kila mtu ana mahusiano na mtu wake.

Kwa upande wa Abela akiulizwa swali  la kuwa na mahusiano na Izzo Bizness anakataa na kusema kuwa wapo kikazi tu na siyo masuala ya mahusiano.

Wawili hao kwa sasa wanafanya vizuri na wimbo ‘Umeniweza’ ambao waliuachia Disemba mwaka jana ambapo inaendelea kubamba masikioni mwa watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *