Timu ya taifa ya Ivory Coast imetolewa kwenye mashindao ya Mataifa ya Afrika yanayonedelea nchini Gabon baada ya kufungwa 1-0 na Morocco katika raundi ya tatu ya kombe hilo.

Ivory Coast ambaye ni bingwa mtetezi wa kombe hilo ameshindwa kulitetea taji lake baada ya kutolewa kwenye hatua ya makundi akiungana na timu kama Argeria pamoja na Gabo ambazo zimetoka hatua hiyo.

Goli pekee liliowaondoa Tembo wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo.

Nayo timu ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo imeitandika Togo kwa mabao 3-1 na hivyo kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara kwa kundi C kwa alama 7 huku Moroco wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Moroco na Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo wanafuzu katika kundi hilo la huku Ivory Coast na Togo zikitupwa nje ya michuano hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *