Aliyekuwa kipa wa Yanga, Simba na timu ya Taifa, Ivo Mapunda anatarajia kufungua kituo cha kuendeleza soka kwa vijana walio chini ya miaka mitano hadi 18 maeneo ya Kitunda Mwanang’ati, Ilala Dar es Salaam ifikapo Novemba 26 mwaka huu.

Ivo Mapunda amesema ameona umuhimu wa kuwafundisha watoto misingi ya soka wangali wadogo.

Pia Ivo ameomba ushirikiano kwa wazazi wote wa Kitunda kwa kuwaruhusu na kuwaleta watoto wao kujifunza soka.

Taratibu za kujiunga na kituo hicho zinapatikana siku ya uzinduzi kwa kushirikiana na serikali ya mtaa.

Ivo Mapunda ni miongoni mwa wachezaji wa Tanzania ambao wamecheza soka kwa mafanikio makubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *