Aliyekuwa kipa wa Taifa Stars, Ivo Mapunda anatarajia kujiunga na klabu ya ligi kuu ya Kenya, AFC Leopards kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika mkataba wake na timu ya Azam Fc ya jijini Dar es Salaam.

Golikipa huyo ambaye aliwahi kucheza kwenye ligi hiyo ya Kenya akiwa na timu ya Gor Mahia inayoshiriki ligi kuu nchini humo kabla ya kurejea Tanzania na kusaini Simba SC ya Jijini Dar es Salaam na kucheza kwa misimu miwili na nusu.

Ivo aliwahi kushinda mataji ya ligi kuu Tanzania Bara akiwa na Yanga  pamoja na ligi kuu nchini Ethiopia wakati akichezea St.George.

Ivo Mapunda anaweka rekodi ya goli kipa wa kwanza kucheza timu zote kubwa za ukanda wa Afrika Mashariki ambapo aliwahi kucheza Yanga SC, Simba SC na Azam FC za Tanzania, St George ya Ethiopia, Gor Mahia na sasa FC Leopards za Kenya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *