Watu 39  wameuawa na wengine 69 wamejeruhiwa katika shambulio la klabu ya burudani mjini Istanbul nchini Uturuki wakati wakisherehekea mwaka mpya.

Mtu mmoja asiyefahamika aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakiburudika katika mkahawa wa Reina saa saba usiku.

Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.

Baadhi yao iliwabidi kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia katika mgahawa huo.

Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika wa shambilo hilo hajakamatwa bado.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *