Waimbaji wa muziki wa Taarab nchini, Isha Mashauzi na Leyla Rashid wanatarajia kupambana katika ukumbi wa Dar Live Oktoba 22 mwaka huu.

Mratibu wa onyesho hilo Hajji Mabovu amesema bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.

Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka.

Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.

Wawili hao ni miongoni mwa wasanii wa taarab wanaofanya vizuri kwasasa kutoka na uimbaji wao kwenye soko la muziki wa taarab.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *