Mwanamuziki nyota wa taarab, Isha Mashauzi amesema kuwa anatarajia kufunga mwaka na kufungua kwa nyimbo yake mpya inaiyotwa ‘Kiss Me’.

Isha Mashauzi amesema amekuwa kimya kwa muda mrefu hivyo nyimbo hiyo inaweza kumrudisha kuwa karibu na mashabiki zake ambao walikuwa wanakosa radha zake kama ilivyokuwa apo awali.

Mashauzi ameongeza kwa kusema kuwa nyimbo hiyo ipo kwenye viwango vya hali ya juu na mashabiki watafurahia kazi hiyo.

Nyimbo hiyo imerekodiwa kwenye studio za Sophia Records zilizopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Mkali huyo ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa taarab hapa nchini ambaye amejizolea umaarufu mkubwa katika tasnia hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *