Kuna msemo wa hekima ya hali ya juu kabisa unasema: Ukitaka kudhihirisha aibu ya mwenzako basi kwanza dhihirisha aibu zako.

Kwa bahati mbaya sana, msanii na mkongwe wa Bongo Fleva, Madee Ali hakuikumbuka hekima hii alipokuwa anahojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo na akaamua kuitoa hadharani aibu ya staa mwenzake MB Dog.

madee

Ingawa yawezekana isionekane kuwa ni jambo kubwa sana lakini ni makosa na ni muhimu sana makosa kurekebishwa yakiwa katika sehemu ya chini sana kwasababu huenda yakiachwa yakajenga uadui zaidi.

Wasanii ni watu ambao mara nyingi hupenda kuzungumzia maisha ya wenzao bila ya kujali athari zinazoweza kujitokeza na mashabiki wameendelea kuvutiwa zaidi na stori tata ambazo huzua majibizano baina ya wasanii na mashabiki wao.

Madee, yawezekana akaona, mbona wengi wanafanya hivi na huenda hata yeye aibu zake zilishawahi kuwekwa hadharani na hakujali lakini ni muhimu sana kutambua kuwa ni makosa makubwa sana kudhihirisha jambo la fedheha la mwenzako.

Madee Ali kwenye mahojiano hayo alizungumzia tukio lililotokea (miaka ya nyuma) kwenye studio za Bongo Records zilizo chini ya producer P-Funky ambapo yeye na mshkaji wake, MB Dog walishindwa kurekodi nyimbo yao kutokana na sababu (aibu) ambayo Madee aliiweka wazi kwenye mahojiano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *