Staa wa masauti na kiongozi wa Malaika Band, Christian Bella kwa mara nyingine tena amethibitisha kuwa yeye ni mkali wa jukwaa na huenda hapa nchini hana mpinzani kwa wanamuziki wa dansi kwa sasa.

Ushahidi wa hilo umekuja baada ya kufanikiwa kutunzwa pesa taslim takribani milioni 15 za kitanzania kwenye shoo ya siku moja.

Bella alikusanya ‘mpunga’ huo baada ya ku-perform kwenye onyesho la THE BLACK TIE lililofanyika kwenye ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam, siku ya Jumamosi.

Mpaka sasa, Bella ndiye staa wa dansi nchini Tanzania mwenye rekodi ya kutunzwa pesa nyingi zaidi awapo jukwaani.

Licha ya Tanzania kuwahi kutembelewa na wasanii wengi wakubwa wa muziki wa dansi kutoka Congo akiwemo Kanda Bongoman, Bozi Boziana, Koffi Olomide n.k lakini mpaka sasa HAKUNA aliyefanikiwa kufikia rekodi ya kutunzwa pesa nyingi zaidi ya 15m akiwa juk

Christian Bella aki 'SUNDA' pesa alizotunzwa kwenye usiku wa THE BLACK TIE
Christian Bella aki ‘SUNDA’ pesa alizotunzwa kwenye usiku wa THE BLACK TIE

waani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *