Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja na muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya wanatarajia kukutana kwenye show moja itakayofanyika mkoani Kilimanjaro.

Mastaa hao ambao walikuwa wapenzi siku ya nyuma wanatarajia kuwepo kwenye show hiyo iliyoandaliwa mkoani humo.

Pia Katika show hiyo mastaa kibao watakuwepo na watatoa burudani lakini wengine wakikutana na mashabiki zao huku wakila bata pamoja.

Katika tukio ambalo wengi wanalisubiria zaidi ni kuwaona mastaa wawili ambao waliwahi kuingia kwenye maisha ya ndoa lakini baada ya muda wakaacha.

Ni muda mrefu sasa tangu watu kuwaona pamoja Dogo Janja na Irene Uwoya kwenye tukio moja baada ya kuachana kwao, sasa katika show hiyo ambayo imeandaliwa na Serengeti lite itawakutanisha mastaa hao na mashabiki wao wana nafasi ya kwenda kukutana nao Hugo Garden Moshi.

Mastaa wengine ambao watakuwepo kwenye show hiyo ni kama Rayvanny, Nandy, Urban Queens

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *