Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Irene Uwoya ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwachana wasanii wenzake kutumia vyombo vya habari kwa kutangaza kuwa walilipwa pesa zao za kampeni kipindi cha uchaguzi mwaka 2015.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Uwoya ameandika amesema kuwa kitendo hicho ni kujishushia heshima na kutaka vitu vingine vibaki kwa wanaohusika tu sio lazima kuongea kila kitu maana watu wanatamani muda mwingine kusikia vitu ambavyo wanahisi vina faida na sio kila saa kuongelea mambo ya chama. 

Uwoya aliandika “Kuna vitu vinaboa sana, kweli kada mzima wa CCM unasimama hadharani unasema tulilipwa kufanya ‘campaign’ ?, hata kama lakini unafundisha nini jamiii?. Unafundisha jamiii kwamba yote tuliyoongea kuhusu CCM hatukuyamanisha ni kwasababu tulilipwa? unaiambia jamiii ulikuwa mnawadanganya sababu mlilipwa?”.

Pia Uwoya amewashauri wenzake wajifunze kunyamaza muda mwingine kama hakuna ulazima wa kuongea maana wanaweza kuhisi wanajenga kumbe ndiyo wanaharibu kabisa.

 “Embu tufanye kazi zinazotuhusu jamanii, ‘Nigeria’ wenzetu sasa wako ‘Hollywood’ wanaigiza huko sisi hata ‘Nigeria’ kwenyewe bado hatuja pasua”.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *