Irene Uwoya atoa shavu kwa vijana kuigiza tamthilia yake ‘Drama Queen’

2
526

Muigizaji nyota wa Bongo movie, Irene Uwoya amesema kuwa ametoa nafasi kwa vijana wawili kuigiza katika Tamthilia yake mpya ya ‘Drama Queen’ itakayotoka mwishoni mwa mwaka huu.

Mwigizaji amesema kuwa ameamua kuandaa tamthilia kutokana na runinga nyingi nchini kuhitaji tamthilia kutokana na waigizaji wengi kubezi kwenye movie pekee.

Uwoya ametoa nafasi kwa vijana wapya wawili kushiriki katika tamthilia hiyo itakayotoka mwishini mwa mwaka huu.

Kupitia ukarasa wake wa Instagram Irene Uwoya ameandika “Drama Queen tunatafuta wa baba wawili kwenye tamthilia yetu, ambaye yupo tayari apige namba hii 0719087622,”.

Irene Uwoya ni muigizaji nyota wa filamu za kibongo ambaye amejizolea umaarufu kutokana na uigizaji wake kwenye filamu tofauti kama vile Dj Beni na nyingine kibao.

LEAVE A REPLY