Kampuni ya Apple imezindua toleo jipya la simu zake ‘iPhone 7’ ambayo inatumia earphone zisizo na waya ‘wireless earphones’.

Simu hiyo ya iPhone 7 badala yake itatumia teknolojia ya Apple ya lightning ambayo itawezesha mtu kutumia tundu moja kuunganisha simu na vifaa vingine.

iphon

Hatua hiyo huenda ikawaudhi baadhi ya wateja ambao sasa watahitajika kununua kifaa unganishi yaani adapter ndipo waweze kutumia visikizia sauti.

Kampuni hiyo ya Marekani ilizindua simu hiyo mpya katika hafla iliyofanyika mjini San Francisco nchini Marekani.

ipho

Hii imejiri baada ya kipindi cha mwaka mmoja cha kushuka kwa mauzo ya simu za iPhone na kupungua kwa sehemu inayodhibitiwa na kampuni hiyo sokoni.

Uzinduzi wa simu hizo umetokea siku chache baada ya Tume ya Ulaya kuamua Apple inafaa kulipa €13bn (£11bn) kama malimbikizi ya kodi kwa Ireland uamuzi ambao Apple imekata rufaa.

Kisikizia sauti cha 3.5mm kilivumishwa sana na vicheza muziki vya Walkman vya kampuni ya Sony lakini kilitumiwa mara ya kwanza katika redio zilizotengenezewa Japan mwaka 1964.

Apple imesema inataka kuacha kutumia viunganishi na vifaa vingine vya zamani kabla ya wapinzani wake.

Moto Z ya Lenovo na vifaa vingine vya LeEco, ya China vilizinduliwa bila tundu la kisikizia muziki hicho cha 3.5mm mapema mwaka huu.

Apple inasema simu hizo  zinaweza kukaa na chaji kwa muda wa saa tano na kifaa chake cha kuhifadhia kinawezesha mtu kutumia kwa hadi saa 24.

iPh

Bei ya iPhone 7 itakuwa kuanzia £599 hadi £799, kwa kutegemea uwezo wake wa kuhifadhi data. Kwa iPhone 7 Plus ni kuanzia £719 hadi £919.

Bei ya kwanza sokoni kwa iPhone 6S ilikuwa £539 na iPhone 6S Plus ilikuwa £619, ingawa uwezo wake wa kuhifadhi data ulikuwa chini.

Simu hizo zilizozinduliwa na kampuni ya Apple ambayo ni iPhone 7 zitaanza kuuzwa kuanzai tarehe 16 Septemba mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *