Mwanamuziki wa Bongo fleva, Inspekta Haroun amesema albamu yake mpya inakaribia kuingia sokoni hivi karibuni baada ya kufanya maandalizi ya kutosha.

Inspekta amesema albamu hiyo itakuwa na nyimbo 14 ambazo amerekodi na maproducer tofauti tofauti ili kupata ladha tofauti ya muziki.

Inspekta maarufu kama Babu amesema “Mimi nachotaka mashabiki wangu wajue Inspekta bado napambana kila siku kwa ajili yao,” alisema Inspekta. “Albamu mpya ipo katika hatua za mwisho, tayari nimerekodi ngoma nyingi na albamu itakuwa na nyimbo 14,”

Mwanamuziki hyuo aliongeza kwa kusema “Msanii huwezi kuishia kuachia single tu, msanii ni albamu. Kwa hiyo mimi nachoweza kusema wasanii tufanye albamu kwa sababu albamu ndio heshima ya msanii,”

Pia Inspekta alisema wimbo kama ‘Masharubu za Babu’ utakuwepo kwenye albamu hiyo ambayo ataisambaza mwenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *