Maelfu ya watu nchini India wameandamana kupinga hatua ya serikali ya nchi hiyo kusitisha matumizi ya noti za rupia 500 na 1,000.

Watu wameendelea kukaa foleni katika benki wakitaka kubadilisha noti hizo zilizositishwa ili kupata noti mpya.

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ametetea uamuzi huo akisema hatua hiyo itasaidia kukabiliana na ulaji rushwa.

Wiki iliyopita, upinzani ulikwamisha shughuli bungeni na kumtaka Modi kuomba radhi kwa sababu ya hatua hiyo.

Mawaziri wakuu wa majimbo ya Bihar na Orissa wamekataa kuunga mkono maandamano hayo wakisema juhudi za Modi za kukabiliana na ufisadi zinafaa kuungwa mkono.

Maandamano yamefanyika katika miji ya Lucknow, Kolkata, na Bangalore wakipinga hatua hiyo ya serikali.

Takriban 90% ya shughuli zote za kibiashara hufanywa kwa pesa taslimu na watu wengi huwa hawana akaunti benki.

Noti zilizositishwa zilijumuisha 86% ya pesa zilizokuwa zinatumiwa katika uchumi wa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *