Serikali ya India imetangaza nia ya kutuma wataalamu wake kufanya uchunguzi wa urefu mlima mrefu zaidi duniani, mlima Everest kwa mara ya pili ili kupima endapo urefu wake ulipungua.

Mpango huo wa India umekuja kufuatia kushuka kwa urefu wa mlima Himalaya kufuatia tetemeko la ardhi la mwaka 2015 lililotokea nchini Nepal.

Mtafiti mkuu wa India, Swarna Subba Rao amesema kuwa timu ya watafiti itatumwa kwaajili ya kazi hiyo ndani ya muda wa miezi miwili.

Hata hivyo maafisa wa Nepal, wameliambia shirika la habari la BBC kuwa bado hakuna makubaliano yaliyofikiwa kwaajili ya kuwaruhusu watafiti wa India kuingia nchini humo kufanya utafiti huo.

Urefu wa mlima huo ambao unatambulika kimataifa ni 8,848m (29,028ft), ambao ulitokana na utafiti uliofanywa na wataalamu wa India yapata miaka 62 iliyopita.

Hata hivyo mkuu wa idara ya utafiti wa kijiografia wa Nepal,

Ganesh Bhatta, amekanusha kufikiwa kwa makubalino hayo na kudai kuwa nchi yake inajipanga kufanya utafiti wake.

Utafiti huo unaweza kuchukua siku 45 hadi kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *