Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa mpaka sasa kikosi cha Polisi kinaendelea na kazi yake wilayani Kibiti.

Kamanda Sirro amesisitiza watu wanaofanya mauaji na utekaji lazima wapatikane na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

 (IGP)  Sirro amesekuwa kuwa katika suala hilo Watanzania wanataka majibu hivyo na yeye tayari ameshatoa maelekezo kwa vikosi vyake na tayari vipo kazini huku akiwaomba wananchi hao waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili waweze kufanikisha kuwakamata watu hao.

“Watanzania wanataka majibu, maelekezo yameshatolewa na vyombo vyetu vinafanya kazi kwa hiyo nisema tu kwamba wananchi waendelee kutupa ushirikiano, tunajua tatizo lipo na lazima tupate majibu.

Pia amesema kuwa “tuna team yetu ya kutosha na askari wa kutosha wanafanya kazi hiyo, kwa hiyo porojo porojo zingine mimi sina katika suala la Kibiti iliyobakia ni kazi tupate majibu, wanaofanya hivyo vitendo wapelekwe kwenye vyombo vya sheria ‘full stop’.

Kauli hiyo ya Sirro imekuja kufuatia watu kuhoji kuendelea kwa mauaji ya raia wilani humo hali ambayo inazua taaruki kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *