Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amewataka Makamishna wastaafu kuendeleza elimu ya polisi jamii pamoja na kutoa msaada wowote utakaohitajika kwa jeshi la hilo.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za kuwaaga makamishna wastaafu zilizofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Polisi.

Makamishna walioagwa ni pamoja na Paul Chagonja, Hamdan Omar Makame na Kenneth Kaseke, ambapo amesema kuwa kazi waliyofanya wastaafu hao ni kubwa lakini kustaafu kwao sio mwisho wa kutumika katika jeshi la polisi.

Kwa upande wake, Paul Chagonja ambaye alikuwa Kamishna wa Oparesheni na mafunzo kwa muda mrefu amewaasa Maofisa na Askari kuendeleza tamaduni na maadili ya Polisi pamoja na kufanya kazi kwa weledi.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama, Mkurugenzi wa Takukuru Kamishna, Valentino Mlowola, IGP Mstaafu Said Mwema, DCI Mstaafu, Robert Manumba na Kamishna Mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Suleiman Kova pamoja na maofisa na Askari Polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *