Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amemteua Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa kuwa msemaji mpya wa jeshi hilo akichukua nafasi ya Kamishina Msaidizi, Advera John Bulimba ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Uteuzi wa Mwakalukwa unatajwa kuwa moja ya harakati za IGP Siro kulifanyia mabadiliko jeshi hilo, katika kuboresha utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kujizatiti na mapambano ya uhalifu.
Kabla ya uteuzi huo, Kamishina Msaidizi Mwakalukwa amelitumikia Jeshi la Polisi kwa nafasi na nyadhifa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kamanda wa Oparesheni wa mikoa mbalimbali pamoja na ngazi zingine za utumishi wa juu.