Baada ya  mauaji ya Mwenyekiti wa Kitongoji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi kilichopo Kata ya Mchukwi wilayani Kibiti katika Mkoa wa Pwani, IGP Simon Sirro ametembelea kijijini hapo kutoa pole kwa wafiwa.

IGP Sirro amewataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo akiwataka kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.

Hiyo ni safari ya pili kwa IGP, Simon Sirro kutembelea wilayani humo toka ateuliwe kuwa mkuu wa jeshi la Polisi nchini.

IGP Simon Sirro akiangalia nyumba ya afisa mtendaji iliyochomwa moto na watu wasiojulikana wilayani Kibiti.
IGP Simon Sirro akiangalia nyumba ya afisa mtendaji iliyochomwa moto na watu wasiojulikana wilayani Kibiti.

Viongozi hao walipigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Mauji hayo ni muendelezo wa matukio yanayotokea katika wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga mkoani Pwani ambapo watu zaidi 30 wameuawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *