Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mange Kimambi.

Kamanda Sirro ameendelea kusema kuwa jeshi la polisi linashughulikia suala hilo kwa makini zaidi.

IGP Sirro amesema hayo jana alipokuwa0 Iringa kwenye ziara ambapo amesema jeshi la polisi linatambua uvunjifu wa sheria ya makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada huyo maarufu mitandaoni ambaye amekuwa mkosoaji wa mambo mbalimbali na kutoa machapisho ambayo serikali inaona ni ya matusi na kashfa kwa serikali na viongozi wake.

IGP Sirro amesema kuwa kwa sasa hawawezi kuweka wazi ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya mwanadada huyo ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani

Mbali na hilo  IGP Sirro amesema jeshi hilo halitawavumilia maafisa wa polisi na askari wanaowasaidia watu wanaofanya unyanyasaji kwa watoto kwa kuwafanyia vitendo vya ubakaji na ulawiti ili kukwepa mkono wa sheria.

Pia Sirro amewataka wananchi wanaohisi kutotendewa haki katika kushughulikia makosa ya aina hiyo kupeleke malalamiko kwa wakuu wa mikoa na viongozi wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *