Aliyekuwa mshindi wa shindano la Big Brother 2014, Idris Sultan amechambua tabia za wasanii watatu wa Bongo fleva, Alikiba, Diamond na Ommy Dimpoz.

Idris ambaye pia ni mchekeshaji na mtangazaji wa radio, amewa­chambua wasanii hao kitabia na kueleza kile ambacho kinaweza kuwafanya wapatane.

Mchekeshaji huyo amesema kuwa bifu la Diamond, Kiba na Ommy Dimpoz ina­tokana na kila mtu kujiona kuwa ni bora zaidi ya mwenzake.

alikiba

Amesema kuwa Kiba ni mtu mwenye majigambo, siku zote anaamini kila anach­okiweza yeye hakuna mwingine anayeweza kuwa juu, ikitokea amezidiwa basi ishu ya majigam­bo ndipo inapoanzia na kujikuta akikosana na wenzake.

Pia Dimpoz ni mtu mvivu sana, yaani huwa hapendi kujibidiisha katika maendeleo yake hadi asu­kumwe, hivyo tabia hii mimi naona kama ndiyo kisa kinachosababi­sha kushindwa kufanikisha mam­bo yake mengi na mwisho wa siku anajikuta akiishia kugombana na wenzake.

diamond-ommy

Kwa upande wa Diamond amesema kuwa anamuona mchapaka­zi sana na anapenda maendeleo ya haraka kiasi kwamba akiona kama kuna mtu anataka kuremba mbele yake huwa hakawii kumpu­uza huku akiendelea kufanya mambo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *