Mchekeshaji, Idris Sultan ameteuliwa kuwa Balozi wa Global Peace Foundation, nchini Tanzania ambapo atawakilisha katika matawi 25 ya mikutano mbalimbali duniani.

Mkurugenzi wa Global Peace Foundation, Martha Nghambi amesema wamemteua  Idris kwa sababu tayari ana sifa za kutuwakilisha Watanzania, hivyo anaweza ni kijana ambaye anaweza kuwafikia watu wengi zaidi.

Picha kwa hisani ya Global Publishers
Picha kwa hisani ya Global Publishers

Kwa upande wake Idris amesema kuwa amepokea kwa shangwe kuteuliwa kuwa balozi wa amani nchini na kuwakilisha vijana wa Kitanzania katika mikutano mbalimbali itakayofanyika duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *