Mchekeshaji maarufu nchini, Idris Sultan amesema kuwa hana tatizo na aliyekuwa mpenzi wake Wema Sepetu na mara kwa mara wanawasiliana kama kipindi cha nyuma.

Idris amesema kuwa huzungumza na ex wake huyo mara chache kwa sasa lakini hawana tatizo lolte wapo kama washikaji.

Mchekeshaji huyo amesema kuwa “Unajua sipendi unafiki nikasema ‘ahh tunaongeaga, mbona washkaji tu tuko peace sana’ hapana sio kihivyo,” amesema Idris.

Ameongeza kwa kusema “Unakuta ni mara moja moja tu, unakuta hebu leo kuna ka mada fulani mmoja kaamua tu kaposti kitu fulani, mmoja kaamua aamshie humo kwahiyo unakuta na mimi ngoja niongee, kwahiyo sio maaadui, ninachoweza kusema sio maadui.”

Idris na Wema walikuwa na uhusiano maarufu ambao ulikuwa ukivunjika na kurejea tena mara kwa mara.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *