Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni, Iddy Azzan amefunguka kwa kusema kuwa amezungukwa na maadui wengi baada ya kutuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Idd Azzan amesema kuwa watu wanaweza kusema lolote baya juu yake kwani ni muda mrefu tangu ameanza kuzungumziwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Mbunge huyo mstaafu amsema kuwa “Mimi tangu nianze kuzungumzwa, sijaanza leo, wanasikiliza kwenye mitandao ya kijamii, hawajui nina maadui wangapi ambao wananizunguka, utakuta mtu  ananitaja kwa chuki zake binafsi ambazo kuthibitisha hawezi.

Azzan amesema polisi walifika nyumbani kwake na kupekuwa, lakini hawakukuta kitu chochote, hivyo anasubiri baadae watamwambia kitu gani.

Idd Azzan ni miongoni mwa watu waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanahojihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya ambao walitakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi Ijumaa iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *