Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan amesema kuwa tuhuma kwamba anahusika na biashara ya dawa za kulevya zilianza toka mwaka 2013.

Azzan amesema hayo baada ya kutajwa katika orodha ya watu 65 wanaotakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kesho kuhusiana na biashara ya dawa za kulevya.

Mbunge huyo wa zamani wa Kinondoni amesema kuwa “Sasa mimi sitaki kuzizungumzia kwa sababu sijui kwanza nilichoitiwa, na hizo tuhuma kwangu zilishatoka tangu 2013 na baadhi ya viongozi wa CCM walisema na zilichukuliwa hatua kipindi kile, kwa hiyo siwezi kusema chochote juu ya hilo kwa kweli”.

Alipoelezwa kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amelitaja jina lake kwenye orodha ya watu wanaohusishwa na biashara ya dawa za kulevya ambao wanatakiwa kuripoti katika Kituo Kikuu cha Polisi, Azzan alijibu: “ Basi aende akaseme vizuri.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa “Kama ningekuwa nafanya hiyo biashara, nafikiri ingekuwa ni rahisi kunikamata na kuniweka ndani, lakini tuache kama ilivyo keshokutwa (kesho) ndiyo nitajua na hapo ndiyo nitasema kitu, lakini kwa sasa tuliache tu.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *