Baaada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwataka wahusika wa madawa ya kulevya kulipoti kituo kikuu cha polisi leo hatimaye baaadhi ya wathumiwa hao wamewasili kituo hapo.

Waliowasili leo katika kituo kikuu ‘Central’ ni mbunge wa zamani wa Kinondoni Iddi Azzan, bosi wa Sea Cliff pamoja na mfanyabiashara wa maduka ya nguo Hussein Pamba Kali na wengine ambao siyo watu maarufu.

Katika orodha hiyo ya watu 65 waliotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya wametakiwa kufika leo kituoni hapo kwa ajili ya mahujiano kuhusu suala hilo.

Manji pamoja na Askofu Gwajima waliripotia kituoni hapo siku ya jana na na kufanyiwa mahojiano juu ya suala hilo linalobeba vichwa vya habari siku hizi.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanzisha suala hilo ili kudhibiti watumiaji na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *