Baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza mwezi Disemba, mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amesema kuwa ameliteka soka la Uingereza kwa muda mfupi toka ajiunge akitokea Paris Saint-German.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa hana malengo binafsi yaliyobakia kwake badala yake ameelekeza nguvu na akili zake kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwasasa.

Lakini Ibrahimovic amesisitiza kuwa lengo lake kuu ni kuisaidia United kuendeleza mwendo wao wa ushindi wa mechi tisa katika michuano yote, ligi ikiwa kipaumbele chake kikuu.

Mshambuliaji huyo aliuambia mtandao wa United: “La! Sifukuzii mtu yeyote bali nafukuzia taji la ligi kuu  msimu huu.

Manchester Uinted inakabiliwa na mechi  dhidi ya Liverpool, na Ibrahimovic ameweka bayana kuwa lengo lao kuu ni kupunguza pengo la pointi dhidi ya timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *