Manchester United wamepata alama tatu muhimu kwenye kundi A baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Zorya Luhansk kwenye mechi ya ligi ya Europa iliyofanyika katika uwanja wa Old Trafford.

Zlatan Ibrahimovic alifunga bao la pekee dakika ya 69, baada ya Wayne Rooney kupiga shuti na kugonga mwamba wa goli na Zlatan kumalizia.

United walitawala mchezo huo ingawa Sergio Romero alihitajika kufanya kazi ya ziada kuzipita mashuti ya Paulinho muda mfupi kabla ya Ibrahimovic kufunga.

Mashetani hao Wekundu walitarajiwa kufanya vyema Europa League lakini walianza kampeni yao kwa kulazwa 1-0 na klabu ya Feyenoord ya Uholanzi mechi yao ya kwanza.

United sasa wanashika nafasi ya tatu katika kundi hilo A wakiwa na alama sawa na Feyenoord na moja nyuma ya viongozi Fenerbahce wa uturuki ambao watacheza Old Trafford 20 Oktoba.

Manchester United wanatarajia kucheza mechi ya ligi kuu nchini Tanzania dhidi ya Stoke City katika uwanja wa Old Trafford.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *