Baada ya kufikia makubalianao ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Manchestr United, mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic anatarajiwa kujiunga na klabu ya LA Galaxy inayoshiriki ligi kuu ya Marekani Major League Soccer.

Taarifa za kujiunga na LA Galaxy ambayo wamepita nyota kadhaa wa soka duniani wakiwemo David Beckham na Frank Lampard zimekuja ikiwa ni chini ya masaa 24 tangu nyota huyo wa Sweden atangaze kumalizana na United.

Ibrahimovic alijiunga na Manchester United mwaka 2016 akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Paris St-German ya Ufaransa. Kabla ya kuomba kuondoka United Zlatan alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 ameichezea United mechi 53 akifanikiwa kufunga mabao 29 huku akiisadia timu hiyo kuibuka na ubingwa wa EUROPA League msimu uliopita.

Mfungaji huyo wa muda wote wa Sweden ameishukuru klabu ya Manchester United ambayo hajaichezea kwa muda wa kutosha msimu huu kutokana na kurejea kutoka kwenye majeruhi yaliyomweka nje kwa muda mrefu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *