Mshambuliaji wa Manchester united, Zlatan Ibrahimovic amesema Wayne Rooney ni mchezaji bora na anastahili heshima zaidi baada ya nahodha huyo wa Uingereza kuvunja rekodi ya ufungaji mabao.

Manchester United walifunga mabao 4-0 dhidi ya Feyenoord kwenye ligi ya Europa iliyochezwa siku ya Alhamisi.

Rooney mwenye umri wa mika 31, alifunga goli la 39 barani Ulaya na kuifanya United kupata alama katika fainali ya hatua ya makundi dhidi ya Zorya Luhansk itakayowafikisha katika timu 32 bora katika ligi ya Europa.

Hii ni kutokana na mchango wa Rooney, ambaye amesalia na goli moja kufikia rekodi ya Sir Bobby Charlton ya magoli 249.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa ‘Tunastahili kumshukuru kwa kuwa michezaji jinsi alivyo kwa kile alichokifanya.

Aliongeza kwa kusema kuwa siwaoni wachezaji wengi kutoka Uingereza walio na taaluma kama yake. Wanastahili kumpa heshima. Kila mtu hupenda kufanya jambo dogo kuwa kubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *